45 Naye heri aliyesadiki; kwa maana yatatimizwa aliyoambiwa na Bwana.
46 Mariamu akasema,Moyo wangu wamwadhimisha Bwana,
47 Na roho yangu imemfurahia Mungu, Mwokozi wangu;
48 Kwa kuwa ameutazamaUnyonge wa mjakazi wake.Kwa maana, tazama, tokea sasaVizazi vyote wataniita mbarikiwa;
49 Kwa kuwa Mwenye nguvu amenitendea makuu,Na jina lake ni takatifu.
50 Na rehema zake hudumu vizazi hata vizaziKwa hao wanaomcha.
51 Amefanya nguvu kwa mkono wake;Amewatawanya walio na kiburi katika mawazo ya mioyo yao;