49 Kwa kuwa Mwenye nguvu amenitendea makuu,Na jina lake ni takatifu.
50 Na rehema zake hudumu vizazi hata vizaziKwa hao wanaomcha.
51 Amefanya nguvu kwa mkono wake;Amewatawanya walio na kiburi katika mawazo ya mioyo yao;
52 Amewaangusha wakuu katika viti vyao vya enzi;Na wanyonge amewakweza.
53 Wenye njaa amewashibisha mema,Na wenye mali amewaondoa mikono mitupu.
54 Amemsaidia Israeli, mtumishi wake;Ili kukumbuka rehema zake;
55 Kama alivyowaambia baba zetu,Ibrahimu na uzao wake hata milele.