45 Akaingia hekaluni, akaanza kuwatoa wale waliokuwa wakifanya biashara,
46 akiwaambia, Imeandikwa, Nyumba yangu itakuwa nyumba ya sala; lakini ninyi mmeifanya kuwa pango la wanyang’anyi.
47 Naye akawa akifundisha kila siku hekaluni. Lakini wakuu wa makuhani, na waandishi, na wakuu wa watu walikuwa wakitafuta njia ya kumwangamiza;
48 wasione la kutenda, kwa kuwa watu wote walikuwa wakiandamana naye, wakimsikiliza.