39 Waandishi wengine wakajibu wakamwambia, Mwalimu, umesema vema;
40 wala hawakuthubutu kumwuliza neno baada ya hayo.
41 Akawaambia, Wasemaje watu kwamba Kristo ni Mwana wa Daudi?
42 Maana, Daudi mwenyewe asema katika chuo cha Zaburi,Bwana alimwambia Bwana wangu,Uketi mkono wangu wa kuume,
43 Hata niwaweke adui zakoKuwa kiti cha kuwekea miguu yako.
44 Basi Daudi amwita Bwana; amekuwaje mwana wake?
45 Na watu wote walipokuwa wakimsikiliza, aliwaambia wanafunzi wake,