46 Akawaambia, Mbona mmelala usingizi? Ondokeni, mkaombe, msije mkaingia majaribuni.
47 Basi alipokuwa katika kusema, tazama, mkutano wa watu, na yule aitwaye Yuda, ambaye ni mmoja wa wale Thenashara, amewatangulia. Akamkaribia Yesu ili kumbusu.
48 Yesu akamwambia, Yuda, wamsaliti Mwana wa Adamu kwa kumbusu?
49 Na wale waliokuwa karibu naye walipoona yatakayotukia, walisema, Bwana, tuwapige kwa upanga?
50 Mmoja wao akampiga mtumwa wa Kuhani Mkuu, akamkata sikio la kuume.
51 Yesu akajibu akasema, Mwe radhi kwa hili. Akamgusa sikio, akamponya.
52 Yesu akawaambia wakuu wa makuhani, na maakida wa hekalu, na wazee, waliokuja juu yake, Je! Mmekuja wenye panga na marungu kama kukamata mnyang’anyi?