1 Akawaita wale Thenashara, akawapa uwezo na mamlaka juu ya pepo wote na kuponya maradhi.
2 Akawatuma wautangaze ufalme wa Mungu, na kupoza wagonjwa.
3 Akawaambia, Msichukue kitu kwa safari yenu, fimbo, wala mkoba, wala mkate, wala fedha, wala mmoja wenu asiwe na kanzu mbili.
4 Na nyumba yo yote mtakayoingia kaeni humo, mpaka mtoke mjini.
5 Na wale wasiowakaribisha, mtokapo katika mji huo, yakung’uteni hata mavumbi ya miguuni mwenu, kuwa ushuhuda juu yao.