15 Na maneno ya manabii yapatana na hayo, kama ilivyoandikwa,
16 Baada ya mambo haya nitarejea,Nami nitaijenga tena nyumba ya Daudi iliyoanguka.Nitajenga tena maanguko yake,Nami nitaisimamisha;
17 Ili wanadamu waliosalia wamtafute Bwana,Na mataifa yote ambao jina langu limetajwa kwao;
18 Asema Bwana, ajulishaye hayo tangu milele.
19 Kwa sababu hiyo mimi naamua hivi; Tusiwataabishe wale waliomgeukia Mungu katika Mataifa;
20 bali tuwaandikie kwamba wajiepushe na unajisi wa sanamu, na uasherati, na nyama zilizosongolewa, na damu.
21 Kwa maana tangu zamani za kale Musa anao watu wahubirio mambo yake; katika kila mji husomwa kila sabato katika masinagogi.