4 Lakini ile jawabu ya Mungu yamwambiaje? Nimejisazia watu elfu saba wasiopiga goti mbele ya Baali.
5 Basi ni vivi hivi wakati huu wa sasa, yako mabaki waliochaguliwa kwa neema.
6 Lakini ikiwa ni kwa neema, haiwi kwa matendo tena, au hapo neema isingekuwa neema.
7 Imekuwaje basi? Kitu kile ambacho Israeli alikuwa akikitafuta hakukipata; lakini wale waliochaguliwa walikipata, na wengine walitiwa uzito.
8 Kama ilivyoandikwa, Mungu aliwapa roho ya usingizi, macho hata wasione, na masikio hata wasisikie, hata siku hii ya leo.
9 Na Daudi asema,Meza yao na iwe tanzi na mtego,Na kitu cha kuwakwaza, na malipo kwao;
10 Macho yao yatiwe giza ili wasione,Ukawainamishe mgongo wao siku zote.