19 Maana utii wenu umewafikilia watu wote; basi nafurahi kwa ajili yenu, lakini nataka ninyi kuwa wenye hekima katika mambo mema, na wajinga katika mambo mabaya.
20 Naye Mungu wa amani atamseta Shetani chini ya miguu yenu upesi.Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo na iwe pamoja nanyi. [Amina.]
21 Timotheo, mtenda kazi pamoja nami, awasalimu, na Lukio, na Yasoni, na Sosipatro, jamaa zangu.
22 Mimi Tertio, niliyeandika waraka huu, nawasalimu katika Bwana.
23 Gayo, mwenyeji wangu na wa Kanisa lote pia awasalimu. Erasto, wakili wa mji, awasalimu, na Kwarto, ndugu yetu.[
24 Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo na iwe pamoja nanyi nyote. Amina.]
25 Sasa na atukuzwe yeye awezaye kuwafanya imara, sawasawa na injili yangu na kwa kuhubiriwa kwake Yesu Kristo, sawasawa na ufunuo wa ile siri iliyositirika tangu zamani za milele,