1 Basi Myahudi ana ziada gani? Na kutahiriwa kwafaa nini?
2 Kwafaa sana kwa kila njia. Kwanza kwa kuwa wamekabidhiwa mausia ya Mungu.
3 Ni nini, basi, ikiwa baadhi yao hawakuamini? Je! Kutokuamini kwao kutaubatili uaminifu wa Mungu?
4 Hasha! Mungu aonekane kuwa amini na kila mtu mwongo; kama ilivyoandikwa,Ili ujulike kuwa una haki katika maneno yako,Ukashinde uingiapo katika hukumu.
5 Lakini, ikiwa udhalimu wetu waithibitisha haki ya Mungu, tuseme nini? Je! Mungu ni dhalimu aletaye ghadhabu? (Nasema kwa jinsi ya kibinadamu.)
6 Hasha! Kwa maana hapo Mungu atawezaje kuuhukumu ulimwengu?