9 Ni nini basi? Tu bora kuliko wengine? La! Hata kidogo. Kwa maana tumekwisha kuwashitaki Wayahudi na Wayunani ya kwamba pia wamekuwa chini ya dhambi;
10 kama ilivyoandikwa, ya kwamba,Hakuna mwenye haki hata mmoja.
11 Hakuna afahamuye;Hakuna amtafutaye Mungu.
12 Wote wamepotoka, wameoza wote pia;Hakuna mtenda mema, la! Hata mmoja.
13 Koo lao ni kaburi wazi,Kwa ndimi zao wametumia hila.Sumu ya fira i chini ya midomo yao.
14 Vinywa vyao vimejaa laana na uchungu.
15 Miguu yao ina mbio kumwaga damu.