25 Ni kama vile alivyosema katika Hosea,Nitawaita watu wangu wale wasiokuwa watu wangu,Na mpenzi wangu yeye asiyekuwa mpenzi wangu.
26 Tena itakuwa mahali pale walipoambiwa,Ninyi si watu wangu,Hapo wataitwa wana wa Mungu aliye hai.
27 Isaya naye atoa sauti yake juu ya Israeli, kusema,Hesabu ya wana wa Israeli, ijapokuwa ni kama mchanga wa bahari, ni mabaki yao tu watakaookolewa.
28 Kwa maana Bwana atalitekeleza neno lake juu ya nchi, akilimaliza na kulikata.
29 Tena kama Isaya alivyotangulia kunena,Kama Bwana wa majeshi asingalituachia uzao,Tungalikuwa kama Sodoma, tungalifananishwa na Gomora.
30 Tuseme nini, basi? Ya kwamba watu wa Mataifa, wasioifuata haki, walipata haki; lakini ni ile haki iliyo ya imani;
31 bali Israeli wakiifuata sheria ya haki hawakuifikilia ile sheria.