28 Kwa maana Bwana atalitekeleza neno lake juu ya nchi, akilimaliza na kulikata.
29 Tena kama Isaya alivyotangulia kunena,Kama Bwana wa majeshi asingalituachia uzao,Tungalikuwa kama Sodoma, tungalifananishwa na Gomora.
30 Tuseme nini, basi? Ya kwamba watu wa Mataifa, wasioifuata haki, walipata haki; lakini ni ile haki iliyo ya imani;
31 bali Israeli wakiifuata sheria ya haki hawakuifikilia ile sheria.
32 Kwa sababu gani? Kwa sababu hawakuifuata kwa njia ya imani, bali kana kwamba kwa njia ya matendo. Wakajikwaa juu ya jiwe lile likwazalo,
33 kama ilivyoandikwa,Tazama, naweka katika Sayuni jiwe likwazalo, na mwamba uangushao;Na kila amwaminiye hatatahayarika.