12 Zikumbukeni ajabu zake alizozifanya;Miujiza yake na hukumu za kinywa chake;
13 Enyi wazao wa Israeli, mtumishi wake,Enyi wana wa Yakobo, wateule wake.
14 Yeye, BWANA, ndiye Mungu wetu;Duniani mwote mna hukumu zake.
15 Likumbukeni agano lake milele,Neno lile aliloviamuru vizazi elfu.
16 Agano alilofanya na Ibrahimu,Na uapo wake kwa Isaka;
17 Alilomthibitishia Yakobo kuwa amri,Na Israeli liwe agano la milele.
18 Akisema, Nitakupa wewe nchi ya Kanaani,Iwe urithi wenu mliopimiwa;