16 Agano alilofanya na Ibrahimu,Na uapo wake kwa Isaka;
17 Alilomthibitishia Yakobo kuwa amri,Na Israeli liwe agano la milele.
18 Akisema, Nitakupa wewe nchi ya Kanaani,Iwe urithi wenu mliopimiwa;
19 Mlipokuwa watu wawezao kuhesabiwa;Naam, watu wachache na wageni ndani yake.
20 Wakatanga-tanga toka taifa hata taifa,Toka ufalme mmoja hata kwa watu wengine.
21 Hakumwacha mtu awaonee;Hata wafalme aliwakemea kwa ajili yao;
22 Akisema, Msiwaguse masihi wangu,Wala msiwadhuru nabii zangu.