21 Hakumwacha mtu awaonee;Hata wafalme aliwakemea kwa ajili yao;
22 Akisema, Msiwaguse masihi wangu,Wala msiwadhuru nabii zangu.
23 Mwimbieni BWANA, nchi yote;Tangazeni wokovu wake siku kwa siku.
24 Wahubirini mataifa habari za utukufu wake,Na watu wote habari za maajabu yake.
25 Kwa kuwa BWANA ni mkuu mwenye kusifiwa sana;Na wa kuhofiwa kuliko miungu yote.
26 Maana miungu yote ya watu si kitu;Lakini BWANA ndiye aliyezifanya mbingu.
27 Heshima na adhama ziko mbele zake;Nguvu na furaha zipo mahali pake.