28 Mpeni BWANA, enyi jamaa za watu,Mpeni BWANA utukufu na nguvu.
29 Mpeni BWANA utukufu wa jina lake;Leteni sadaka, mje mbele zake;Mwabuduni BWANA kwa uzuri wa utakatifu;
30 Tetemekeni mbele zake, nchi yote.Naam, ulimwengu umethibitika usitikisike;
31 Mbingu na zifurahi, nchi na ishangilie;Na waseme katika mataifa, BWANA ametamalaki;
32 Bahari na ivume na vyote viijazavyo;Mashamba na yashangilie na vyote vilivyomo;
33 Ndipo miti yote ya mwituni iimbe kwa furaha,Mbele za BWANA,Kwa maana anakuja aihukumu nchi.
34 Mshukuruni BWANA kwa kuwa ni mwema;Kwa maana fadhili zake ni za milele.