9 Mwimbieni, mwimbieni kwa zaburi;Zitafakarini ajabu zake zote.
10 Jisifuni kwa jina lake takatifu;Na ufurahi moyo wao wamtafutao BWANA.
11 Mtakeni BWANA na nguvu zake;Utafuteni uso wake siku zote.
12 Zikumbukeni ajabu zake alizozifanya;Miujiza yake na hukumu za kinywa chake;
13 Enyi wazao wa Israeli, mtumishi wake,Enyi wana wa Yakobo, wateule wake.
14 Yeye, BWANA, ndiye Mungu wetu;Duniani mwote mna hukumu zake.
15 Likumbukeni agano lake milele,Neno lile aliloviamuru vizazi elfu.