18 Penye Parbari upande wa magharibi, walikuwapo wanne darajani, na wawili huko Parbari.
19 Hizo ndizo zamu za mabawabu; wa wana wa Wakora, na wa wana wa Merari.
20 Na katika Walawi; Ahia alikuwa juu ya hazina za nyumba ya Mungu, na juu ya hazina za vitu vilivyowekwa wakfu.
21 Wana wa Ladani; wana wa Wagershoni waliokuwa wa Ladani; wakuu wa mbari za mababa waliokuwa wa Ladani, Mgershoni; Yehieli.
22 Wana wa Yehieli; Zethamu, na Yoeli nduguye, juu ya hazina za nyumba ya BWANA.
23 Wa Waamramu, wa Waishari, wa Wahebroni, wa Wauzieli;
24 na Shebueli, mwana wa Gershomu, mwana wa Musa, alikuwa mtawala hazina zote.