11 na Azaria akamzaa Amaria; na Amaria akamzaa Ahitubu;
12 na Ahitubu akamzaa Sadoki; na Sadoki akamzaa Meshulamu;
13 na Meshulamu akamzaa Hilkia; na Hilkia akamzaa Azaria;
14 na Azaria akamzaa Seraya; na Seraya akamzaa Yehosadaki;
15 na Yehosadaki akachukuliwa mateka, hapo BWANA alipowachukua mateka Yuda na Yerusalemu, kwa mkono wa Nebukadreza.
16 Wana wa Lawi; Gershoni, na Kohathi, na Merari.
17 Na haya ndiyo majina ya wana wa Gershoni; Libni, na Shimei.