16 Na Maaka mkewe Makiri, akamzalia mwana, akamwita jina lake Pereshi; na jina la nduguye aliitwa Shereshi; na wanawe walikuwa Ulamu, na Rakemu.
17 Na wana wa Ulamu; Bedani. Hao ndio wana wa Gileadi, mwana wa Makiri, mwana wa Manase.
18 Na umbu lake, Hamolekethi, akamzaa Ish-hodu, na Abiezeri, na Mala.
19 Na wana wa Shemida walikuwa Ahiani, na Shekemu, na Liki, na Aniamu.
20 Na wana wa Efraimu; Shuthela, na mwanawe huyo ni Beredi, na mwanawe huyo ni Tahathi, na mwanawe huyo ni Ekada, na mwanawe huyo ni Tahathi;
21 na mwanawe huyo ni Zabadi, na mwanawe huyo ni Shuthela; na Ezeri na Ekadi, ambao watu wa Gathi, wenyeji wa nchi, waliwaua, kwa sababu walishuka ili kuzipokonya ng’ombe zao.
22 Na Efraimu, baba yao, akaomboleza siku nyingi, wakaja nduguze ili kumfariji.