13 Basi sasa, mtazameni mfalme mliyemchagua na kumtaka; tazameni, BWANA ameweka mfalme juu yenu.
14 Kama mkimcha BWANA, na kumtumikia, na kuisikia sauti yake, msiiasi amri ya BWANA, tena kama ninyi, na mfalme anayewatawala, mkimfuata BWANA, Mungu wenu, vema!
15 Bali msipoisikia sauti ya BWANA, mkiiasi amri ya BWANA, ndipo mkono wa BWANA utakuwa juu yenu, kama ulivyokuwa juu ya baba zenu.
16 Na sasa simameni, mkalione jambo hili kubwa, BWANA atakalolitenda mbele ya macho yenu.
17 Leo je! Si mavuno ya ngano? Nitamwomba BWANA, kwamba apeleke ngurumo na mvua; nanyi mtajua na kuona ya kuwa uovu wenu ni mwingi sana, mlioufanya machoni pa BWANA, kwa kujitakia mfalme.
18 Basi Samweli akamwomba BWANA, naye BWANA akapeleka ngurumo na mvua siku ile; nao watu wote wakamwogopa BWANA sana, na Samweli pia.
19 Watu wote wakamwambia Samweli, Utuombee sisi watumwa wako kwa BWANA, Mungu wako, tusije tukafa; maana tumeongeza dhambi zetu zote kwa uovu huu, wa kujitakia mfalme.