13 Toka mwangaza uliokuwa mbele zakeMakaa ya moto yakawashwa.
14 BWANA alipiga radi toka mbinguni,Naye Aliye juu akaitoa sauti yake.
15 Akapiga mishale, akawatawanya;Umeme, naye akawatapanya.
16 Ndipo ilipoonekana mikondo ya bahari,Misingi ya ulimwengu ikafichuliwa,Kwa kukemea kwake BWANA,Kwa mvumo wa pumzi ya puani mwake.
17 Alipeleka kutoka juu, akanishika;Akanitoa katika maji mengi;
18 Akaniokoa na adui yangu mwenye nguvu,Na wale walionichukia;Maana walikuwa na nguvu kuliko mimi.
19 Walinikabili siku ya msiba wangu;Lakini BWANA alikuwa tegemeo langu.