19 Walinikabili siku ya msiba wangu;Lakini BWANA alikuwa tegemeo langu.
20 Akanitoa akanipeleka panapo nafasi;Aliniponya kwa kuwa alipendezwa nami.
21 BWANA alinitendea sawasawa na haki yangu;Sawasawa na usafi wa mikono yangu akanilipa.
22 Maana nimezishika njia za BWANA,Wala sikumwasi Mungu wangu.
23 Maana hukumu zake zote zilikuwa mbele yangu;Na kwa habari za amri zake, sikuziacha.
24 Nami nalikuwa mkamilifu kwake,Nikajilinda na uovu wangu.
25 Basi BWANA amenilipa sawasawa na haki yangu;Sawasawa na usafi wa mikono yangu mbele zake.