26 Kwa mtu mwenye fadhili utakuwa mwenye fadhiliKwa mkamilifu utajionyesha kuwa mkamilifu;
27 Kwake ajitakasaye utajionyesha kuwa mtakatifu;Na kwa mpotovu utajionyesha kuwa mkaidi.
28 Na watu wanaoonewa wewe utawaokoa;Ila macho yako ni juu ya wenye kiburi, uwadhili.
29 Kwa kuwa wewe u taa yangu, Ee BWANA;Na BWANA ataniangazia giza langu.
30 Maana kwa msaada wako nafuatia jeshi;Kwa msaada wa Mungu wangu naruka ukuta.
31 Mungu njia yake ni kamilifu;Ahadi ya BWANA imehakikishwa;Yeye ndiye ngao yaoWote wanaomkimbilia.
32 Maana ni nani aliye Mungu, ila BWANA?Ni nani aliye mwamba, ila Mungu wetu?