30 Maana kwa msaada wako nafuatia jeshi;Kwa msaada wa Mungu wangu naruka ukuta.
31 Mungu njia yake ni kamilifu;Ahadi ya BWANA imehakikishwa;Yeye ndiye ngao yaoWote wanaomkimbilia.
32 Maana ni nani aliye Mungu, ila BWANA?Ni nani aliye mwamba, ila Mungu wetu?
33 Mungu ndiye ngome yangu yenye nguvu;Naye huwaongoza wakamilifu katika njia yake.
34 Huifanya miguu yangu kuwa kama ya kulungu;Na kunisimamisha mahali pangu pa juu.
35 Ananifundisha mikono yangu vita;Hata mikono yangu yaupinda upinde wa shaba.
36 Nawe umenipa ngao ya wokovu wako;Na unyenyekevu wako umenikuza.