35 Ananifundisha mikono yangu vita;Hata mikono yangu yaupinda upinde wa shaba.
36 Nawe umenipa ngao ya wokovu wako;Na unyenyekevu wako umenikuza.
37 Umezifanyizia nafasi hatua zangu,Wala miguu yangu haikuteleza.
38 Nimewafuatia adui zangu, na kuwaangamiza;Wala sikurudi nyuma hata walipokomeshwa.
39 Nami nimewakomesha na kuwapiga-piga wasiweze kusimama;Naam, wameanguka chini ya miguu yangu.
40 Maana umenifunga mshipi wa nguvu kwa vita;Umenitiishia chini yangu walioniondokea.
41 Naam, adui zangu umewafanya wanipe visogo,Ili niwakatilie mbali wanaonichukia.