38 Nimewafuatia adui zangu, na kuwaangamiza;Wala sikurudi nyuma hata walipokomeshwa.
39 Nami nimewakomesha na kuwapiga-piga wasiweze kusimama;Naam, wameanguka chini ya miguu yangu.
40 Maana umenifunga mshipi wa nguvu kwa vita;Umenitiishia chini yangu walioniondokea.
41 Naam, adui zangu umewafanya wanipe visogo,Ili niwakatilie mbali wanaonichukia.
42 Walitazama, lakini hakuna wa kuokoa;Walimwita BWANA, lakini hakuwajibu.
43 Ndipo nikawaponda kama mavumbi ya nchi,Nikawakanyaga kama matope ya njiani, nikawatawanya.
44 Nawe umeniokoa na mashindano ya watu wangu;Umenihifadhi niwe kichwa cha mataifa;Watu nisiowajua watanitumikia.