45 Wageni watanijia wakinyenyekea;Kwa kusikia tu habari zangu,Mara watanitii.
46 Wageni nao watatepetea,Watatoka katika ngome zao wakitetemeka.
47 BWANA ndiye aliye hai;Na ahimidiwe mwamba wangu;Na atukuzwe Mungu wa mwamba wa wokovu wangu;
48 Naam, Mungu anipatiaye kisasi,Na kuwatweza watu chini yangu,
49 Na kunileta nje nitoke kwa adui zangu;Naam, waniinua juu yao walioniinukia;Waniponya na mtu wa jeuri.
50 Basi, BWANA, nitakushukuru kati ya mataifa,Nami nitaliimbia jina lako.
51 Ampa mfalme wake wokovu mkuu;Amfanyia fadhili masihi wake,Daudi na mzao wake, hata milele.