12 Ndipo Zerubabeli, mwana wa Shealtieli, na Yoshua, mwana wa Yehosadaki, kuhani mkuu, pamoja na hayo mabaki yote ya watu, wakaitii sauti ya BWANA, Mungu wao, na maneno ya Hagai nabii, kama BWANA, Mungu wao, alivyomtuma; nao watu wakaogopa mbele za BWANA.