20 Nami nitakuposa kwa uaminifu; nawe utamjua BWANA.
21 Tena itakuwa siku hiyo, mimi nitaitika, asema BWANA; nitaziitikia mbingu, nazo zitaiitikia nchi;
22 nayo nchi itaiitikia nafaka na divai na mafuta; nayo yataiitikia Yezreeli.
23 Nami nitampanda katika nchi kwa ajili yangu mwenyewe; nami nitamrehemu yeye asiyepewa rehema; nami nitawaambia wale wasiokuwa watu wangu, Ninyi ndinyi watu wangu; nao watasema, Wewe ndiwe Mungu wangu.