7 Lakini wao wamelivunja hilo agano kama Adamu; huko wamenitenda mambo ya hiana.
8 Gileadi ni mji wa hao watendao maovu, umetiwa rangi ya damu.
9 Na kama vile makundi ya wanyang’anyi wamwoteavyo mtu, ndivyo kundi la makuhani wauavyo katika njia ielekeayo Shekemu; naam, wametenda mambo maovu sana.
10 Katika nyumba ya Israeli nimeona jambo bovu kabisa; huko uzinzi umeonekana katika Efraimu; Israeli ametiwa unajisi.
11 Tena, Ee Yuda, wewe umeandikiwa mavuno, hapo nitakapowarudisha wafungwa wa watu wangu.