10 Iwapo chuma hakipati, wala mtu hakinoi;Ndipo hana budi kutumia nguvu zaidi. Walakini yafaa kutumia hekima, na kufanikiwa.
11 Nyoka akiuma asijatumbuizwa,Basi hakuna faida ya mtumbuizi.
12 Maneno ya kinywa chake mwenye hekima yana neema;Bali midomo ya mpumbavu itammeza nafsi yake.
13 Mwanzo wa maneno ya kinywa chake ni upuuzi; na mwisho wa usemi wake ni wazimu wenye hatari.
14 Tena, upumbavu huongeza maneno; lakini mwanadamu hajui yatakayokuwako; nayo yatakayokuwa baada yake, ni nani awezaye kumweleza?
15 Kazi yao wapumbavu huwachosha kila mmoja,Maana hajui hata njia ya kuuendea mji.
16 Ole wako, nchi, akiwa mfalme wako ni kijana,Na wakuu wako hula asubuhi!