5 Liko baa nililoliona chini ya jua, nalo ni kama kosa litokalo kwake yeye atawalaye;
6 ya kuwa upumbavu huwekwa mahali pa juu sana, nao wakwasi hukaa mahali pa chini.
7 Mimi nimeona watumwa wamepanda farasi, na wakuu wakienda kwa miguu juu ya nchi kama watumwa.
8 Mwenye kuchimba shimo atatumbukia ndani yake;Na yeye abomoaye boma, nyoka atamwuma.
9 Mwenye kuchonga mawe ataumizwa kwayo;Naye apasuaye miti huona hatari katika hiyo.
10 Iwapo chuma hakipati, wala mtu hakinoi;Ndipo hana budi kutumia nguvu zaidi. Walakini yafaa kutumia hekima, na kufanikiwa.
11 Nyoka akiuma asijatumbuizwa,Basi hakuna faida ya mtumbuizi.