7 Mimi nimeona watumwa wamepanda farasi, na wakuu wakienda kwa miguu juu ya nchi kama watumwa.
8 Mwenye kuchimba shimo atatumbukia ndani yake;Na yeye abomoaye boma, nyoka atamwuma.
9 Mwenye kuchonga mawe ataumizwa kwayo;Naye apasuaye miti huona hatari katika hiyo.
10 Iwapo chuma hakipati, wala mtu hakinoi;Ndipo hana budi kutumia nguvu zaidi. Walakini yafaa kutumia hekima, na kufanikiwa.
11 Nyoka akiuma asijatumbuizwa,Basi hakuna faida ya mtumbuizi.
12 Maneno ya kinywa chake mwenye hekima yana neema;Bali midomo ya mpumbavu itammeza nafsi yake.
13 Mwanzo wa maneno ya kinywa chake ni upuuzi; na mwisho wa usemi wake ni wazimu wenye hatari.