5 tena, haikuliona jua wala kulifahamu; basi, hii imepata kustarehe kuliko yule;
6 naam, ajapoishi miaka elfu mara mbili, asijiburudishe kwa mema; je! Wote hawaendi mahali pamoja?
7 Kazi yote ya binadamu ni kwa kinywa chake,Walakini hata hivyo nafsi yake hashibi.
8 Kwa maana mwenye hekima hupata faida gani kuliko mpumbavu? Au maskini ana nini kuliko yeye ajuaye kwenda mbele ya walio hai?
9 Heri kuona kwa macho,Kuliko kutanga-tanga kwa tamaa.Hayo nayo ni ubatili, na kujilisha upepo.
10 Na awe kitu cho chote, aliitwa jina lake zamani za kale, naye amejulikana kuwa ndiye mwanadamu; wala hawezi kabisa kushindana na yeye aliye na uwezo kuliko yeye mwenyewe.
11 Basi, kwa kuwa kuna mambo mengi yaongezayo ubatili, mwanadamu hufaidiwa nini?