5 Heri kusikia laumu ya wenye hekima,Kuliko mtu kusikia wimbo wa wapumbavu;
6 Maana kama mlio wa miiba chini ya sufuria,Ndivyo kilivyo kicheko cha mpumbavu.Hayo nayo ni ubatili.
7 Kweli jeuri humpumbaza mwenye hekima,Na rushwa huuharibu ufahamu.
8 Heri mwisho wa neno kuliko mwanzo wake,Na mvumilivu rohoni kuliko mwenye roho ya kiburi.
9 Usifanye haraka kukasirika rohoni mwako,Maana hasira hukaa kifuani mwa wapumbavu.
10 Usiseme, Kwani siku za kale kupita siku hizi?Maana si kwa hekima uulizavyo neno hilo.
11 Hekima ni njema, mfano wa urithi;Naam, nayo ni bora kwao walionao jua.