2 Kwa maana BWANA anairudisha fahari ya Yakobo, kama fahari ya Israeli; maana watekao nyara wamewateka, na kuyaharibu matawi ya mizabibu yao.
3 Ngao ya mashujaa wake imefanywa kuwa nyekundu, watu walio hodari wa vita wamevaa nguo nyekundu sana; magari ya vita yametameta kwa chuma cha pua siku ya kujitengeza kwake, na mikuki inatikiswa kwa namna ya kutisha.
4 Magari ya vita yanafanya mshindo njiani,Yanasongana-songana katika njia kuu;Kuonekana kwake ni kama mienge,Yanakwenda upesi kama umeme.
5 Awakumbuka watu wake wenye heshima;Wanajikwaa katika mwendo wao;Wanafanya haraka waende ukutani;Nacho kitu cha kuwafunika kimewekwa tayari.
6 Malango ya mito yamefunguka, na jumba la mfalme limeyeyushwa.
7 Husabu naye amefunuliwa, anachukuliwa, na wajakazi wake wanalia kama kwa sauti ya hua, wakipiga-piga vifua vyao.
8 Lakini Ninawi tokea zamani amekuwa kama ziwa la maji; ila hata sasa wanakimbia; Simameni! Simameni! Lakini hapana hata mmoja atazamaye nyuma.