5 Awakumbuka watu wake wenye heshima;Wanajikwaa katika mwendo wao;Wanafanya haraka waende ukutani;Nacho kitu cha kuwafunika kimewekwa tayari.
6 Malango ya mito yamefunguka, na jumba la mfalme limeyeyushwa.
7 Husabu naye amefunuliwa, anachukuliwa, na wajakazi wake wanalia kama kwa sauti ya hua, wakipiga-piga vifua vyao.
8 Lakini Ninawi tokea zamani amekuwa kama ziwa la maji; ila hata sasa wanakimbia; Simameni! Simameni! Lakini hapana hata mmoja atazamaye nyuma.
9 Chukueni nyara za fedha;Chukueni nyara za dhahabu;Kwa maana ni akiba isiyoisha,Fahari ya vyombo vipendezavyo.
10 Amekuwa utupu, na ukiwa, na uharibifu; hata moyo unayeyuka, na magoti yanagongana-gongana; viunoni mwote mna utungu, na nyuso za wote zimekuwa nyeupe kwa hofu.
11 Kao la simba li wapi? Na mahali walishapo wana-simba pa wapi, mahali walipotembea simba mume na simba mke na mwana-simba, wala hapana aliyewatia hofu?