24 Haloheshi, Pilha, Shobeki;
25 Rehumu, Hashabna, Maaseya;
26 Ahia, Hanani, Anani;
27 Maluki, Harimu, na Baana.
28 Na watu waliosalia, makuhani, Walawi, mabawabu, waimbaji, Wanethini, na hao wote waliojitenga katika watu wa nchi kwa torati ya Mungu; wake zao, na wana wao, na binti zao, kila mwenye maarifa na akili;
29 wakaambatana na ndugu zao, wakuu wao, nao wakaingia katika laana na kiapo, ya kuwa wataiendea torati ya Mungu, iliyotolewa kwa mkono wa Musa, mtumishi wa Mungu, na kuziangalia, na kuzitenda, amri zote za BWANA, Bwana wetu, na hukumu zake na sheria zake;
30 wala tusiwaoze watu wa nchi binti zetu, wala kuwatwalia wana wetu binti zao;