1 Ikawa, hapo ukuta ulipojengwa, na milango nimekwisha kuisimamisha, na mabawabu, na waimbaji, na Walawi, wamewekwa,
2 ndipo nilimwagiza ndugu yangu, Hanani, pamoja na yule Hanania, jemadari wa ngome, kuwa na amri juu ya Yerusalemu; kwa maana alikuwa mtu mwaminifu huyo, na mwenye kumcha Mungu kuliko wengi.
3 Nikawaambia, Yasifunguliwe malango ya Yerusalemu kabla halijachomoza jua; nao walinzi wangali wakisimama bado, waifunge milango, mkaikaze; kisha wekeni walinzi wa zamu wa hao wakaao Yerusalemu, kila mtu na zamu yake, na kila mtu kuielekea nyumba yake.
4 Basi mji ulikuwa wa nafasi nyingi, tena mkubwa; lakini watu waliomo walikuwa haba, wala nyumba hazijajengwa.
5 Mungu wangu akanitia moyoni mwangu, kwamba niwakusanye wakuu na mashehe, na watu, ili wahesabiwe kwa nasaba.Nikakiona kitabu cha vizazi vya hao waliokwea hapo kwanza, nikaona ya kwamba imeandikwa humo;