16 Je! Chakula hakikukatiliwa mbali mbele ya macho yetu? Naam, furaha na kicheko mbali na nyumba ya Mungu wetu?
17 Mbegu zinaoza chini ya udongo wake; ghala zimeachwa ukiwa; mabanda yamevunjika; kwa maana nafaka imekauka.
18 Jinsi wanyama wanavyougua! Makundi ya ng’ombe yamefadhaika, kwa sababu hawana malisho; naam, makundi ya kondoo yamepata mateso.
19 Ee BWANA, nakulilia wewe;Kwa maana moto umeyala malisho ya nyikani,Na miali ya moto imeteketeza miti yote ya mashamba.
20 Naam, wanyama wa mashamba wanakutwetea wewe;Kwa maana vijito vya maji vimekauka,Na moto umeyateketeza malisho ya nyikani.