4 Yaliyosazwa na tunutu yameliwa na nzige; na yaliyosazwa na nzige yameliwa na parare; na yaliyosazwa na parare yameliwa na madumadu.
5 Levukeni, enyi walevi, mkalie;Pigeni yowe, ninyi nyote mnywao divai;Kwa sababu ya divai mpya;Maana umekatiliwa mbali na vinywa vyenu.
6 Maana taifa limepanda juu ya nchi yangu,Lenye nguvu, tena halina hesabu;Meno yake ni kama meno ya simba,Naye ana magego ya simba mkubwa.
7 Ameuharibu mzabibu wangu; ameuvunja mtini wangu; ameyaambua magamba yake kabisa; ameuangusha chini; matawi yake yamefanywa kuwa meupe.
8 Ombolea kama mwanamwali avaaye maguniaKwa ajili ya mume wa ujana wake.
9 Sadaka ya unga na sadaka ya kinywajiZimekatiliwa mbali na nyumba ya BWANA;Hao makuhani, wahudumu wa BWANA, wanaomboleza.
10 Shamba limeharibika, nchi inaomboleza; maana nafaka imeharibika, divai mpya imekauka, mafuta yamepunguka.