11 Kwake yawe mamlaka milele! Amina.
12 Nimewaandikieni barua hii fupi kwa msaada wa Silwano, ndugu ambaye namjua na kumwamini. Nataka kuwapeni moyo na kushuhudia kwamba jambo hili ni neema ya Mungu kweli. Kaeni imara katika neema hiyo.
13 Jumuiya ya wenzenu walioteuliwa na Mungu hapa Babuloni wanawasalimuni. Vilevile mwanangu Marko anawasalimuni.
14 Salimianeni kwa ishara ya upendo wa Kikristo.Nawatakieni amani nyinyi mlio wake Kristo.