3 Nilipokuwa kwenu nilikuwa dhaifu, natetemeka kwa hofu nyingi.
4 Hotuba zangu na mahubiri yangu sikuyatoa kwa maneno ya kuvutia na ya hekima, bali kwa uthibitisho mwingi na nguvu ya Roho.
5 Nilifanya hivyo kusudi imani yenu ipate kutegemea nguvu ya Mungu, na si hekima ya binadamu.
6 Hata hivyo, sisi tunatumia lugha ya hekima kwa wale waliokomaa kiroho; lakini hekima hiyo si ya hapa duniani, wala si ya watawala wa dunia hii ambao wako katika mkumbo wa kupotea.
7 Hekima tunayotumia ni hekima ya siri ya Mungu, hekima iliyofichika, ambayo Mungu aliiazimia tangu mwanzo kwa ajili ya utukufu wetu.
8 Ni hekima ambayo watawala wa dunia hii hawakuielewa; maana wangaliielewa, hawangalimsulubisha Bwana wa utukufu.
9 Lakini, ni kama yasemavyo Maandiko Matakatifu:“Mambo ambayo jicho halijapata kuyaona,wala sikio kuyasikia,mambo ambayo binadamu hajapata kuyafikiria moyoni,hayo ndiyo Mungu aliyowatayarishia wale wampendao.”