18 Baadhi yenu wameanza kuwa na majivuno wakidhani kwamba sitakuja tena kwenu.
19 Lakini, Bwana akipenda, nitakuja kwenu upesi; na hapo ndipo nitakapojionea mwenyewe, sio tu kile wanachoweza kusema hao wenye majivuno, bali pia kile wanachoweza kufanya.
20 Maana ufalme wa Mungu si shauri la maneno matupu, bali ni nguvu.
21 Mnapendelea lipi? Nije kwenu na fimbo, ama nije na moyo wa upendo na upole?