1 Hatimaye, ndugu zangu, mmejifunza kutoka kwetu namna mnavyopaswa kuishi ili kumpendeza Mungu. Na kweli mmekuwa mnaishi hivyo. Sasa tunawaombeni na kuwasihi kwa jina la Bwana Yesu mfanye vema zaidi.
2 Maana mnayajua yale maagizo tuliyowapeni kwa mamlaka ya Bwana Yesu.
3 Mungu anataka nyinyi muwe watakatifu na mjiepushe kabisa na maisha ya zinaa.
4 Kila mwanamume anapaswa kujua namna ya kuishi na mkewe kwa utakatifu na heshima,
5 na si kwa tamaa mbaya kama watu wa mataifa mengine wasiomjua Mungu.