15 Naam, mpaka hivi leo kila isomwapo sheria akili zao huwa zimefunikwa.
16 Lakini, wakati mtu amgeukiapo Bwana, kifuniko hicho huondolewa.
17 Hapa “Bwana” ni Roho; na pale alipo Roho wa Bwana ndipo ulipo uhuru.
18 Basi, sisi sote ambao nyuso zetu hazikufunikwa, tunaona kama katika kioo, utukufu wa Bwana; tunabadilishwa tufanane zaidi na huo mfano wake kwa utukufu mwingi zaidi. Hiyo ni kazi yake Roho wa Bwana.