12 Kila mtu anamsifu Demetrio; naam, ukweli wenyewe unamsifu. Nasi pia tunatoa ushahidi wetu juu yake, nawe wajua kwamba tunachosema ni kweli.
13 Ninayo bado mengi ya kukuambia, lakini sipendi kuyaandika kwa kalamu na wino.
14 Natumaini kukuona karibuni na hapo tutazungumza ana kwa ana.
15 Nakutakia amani. Rafiki zako wanakusalimu. Wasalimu rafiki zetu wote kila mmoja binafsi.