54 Amemsaidia Israeli mtumishi wake,akikumbuka huruma yake,
55 kama alivyowaahidia wazee wetu,Abrahamu na wazawa wake hata milele.”
56 Maria alikaa na Elisabeti kwa muda upatao miezi mitatu, halafu akarudi nyumbani kwake.
57 Wakati wa kujifungua kwake Elisabeti ulifika, akajifungua mtoto wa kiume.
58 Jirani na watu wa jamaa yake walipopata habari kwamba Bwana amemwonea huruma kubwa, walifurahi pamoja naye.
59 Halafu siku ya nane walifika kumtahiri mtoto, wakataka kumpa jina la baba yake, Zakaria.
60 Lakini mama yake akasema, “Sivyo, bali ataitwa Yohane.”